Habari

Afisa wa Polisi Caroline Kagogo Ajiuwa………………………..

Afisa wa polisi Caroline Kangogo anayetuhumiwa kwa kuwauwa watu wawili amejiuwa.

Inaarifiwa kuwa Kangogo amejiuwa kwa kujipiga risasi nyumbani kwao eneo la nyawa kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Kwa mujibu wa maafisa wa upelelezi wa jinai, Kagongo alifika nyumbani kwao saa kumi na moja alfajiri na kuelekea kwenye bafu ambapo alijipiga risasi kichwani.

Mratibu wa bonde la ufa George Natembeya amethibitisha kisa hicho na kusema ya kwamba Kagongo alipatika kwenye bafu nyumbani kwao

Polisi wamepata simu aliyokuwa akitumia na ambayo itatumika kwa uchunguzi zaidi.