Naibu rais dkt William Ruto amewataka viongozi kuwatumikia wananchi badala ya kujinufaisha wao binafsi.
Ruto amewaonya viongozi dhidi ya mipango ya kuibadilisha katiba kwa ajili ya kujitafutia nafasi za kusalia mamlakani.
Akizungumza mjini Kilifi baada ya kushiriki ibada katika kanisa katoliki la mtakatifu Patrisi, Ruto amesema viongozi wamefumbia macho swala la kudorora kwa uchumi unaowaathiri wananchi na kuangazia swala la mabadiliko ya katiba.
Aidha amesema serikali inajitahidi kuhakikisha miradi iliyoanzishwa inakamilika, akiongeza kuwa hatua hiyo inalenga kuwashirikisha vijana katika ujenzi wa taifa.
Hata hivyo Ruto amesema mradi wa kujenga chuo cha kiufundi katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini utaanza hivi karibuni.
BY ERICKSON KADZEHA