Spika wa bunge la Kitaifa Justin Muturi amewataka wasomi kote nchini kuwa katika mstari wa mbele kusaidia jamii katika kuwa na viongozi wenye maono ili kuwawezesha kujadiliana na kujadilli masuala yanayolizonga taifa kwa njia iliyobora akisema kwa kufanya hivyo taifa litafikia maendeleo yanayostahili.
Muturi amesema makundi mengi ya wasomi hapa nchini yameepuka siasa wakti yanamaoni ju ya chagua bora ambazo zinawezesha kuongoza wapi uongozi bora unajiri.
Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Embu wakati wa warsha ya kila mwaka ya wataalam katika nyanja mbalimbali, amesema kuwa inasikitisha kuona wanaelekeza juhudi zao zaidi ju ya nani atakayewaongoza katika vyama vya wakaazi
Aidha ametoa changamoto kwa wanawake kujitosa katika siasa za ushindani na waache kutegea nyadhifa maalum katika bunge
Vilevile ametoa wito kwa viongozi wanawake walioko kwenye siasa kuwakuza na kuwaonyesha njia wanawake wenza walio na azma sawa..
BY PRESTON WANDERA