Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ametoa wito kwa maasifa wa polisi pamoja na idara ya Mahakama kumaliza kwa haraka kesi za visa vya watu hasa watoto na wanawakekupotea na mwishoe kupatikana wameuwawa mara kwa mara.
Raila amesema watoto na wanawake wengi wamepoteza maisha yao kwenye mikono ya watu ambao wanafaa kuwalinda.
Hata hivyo kinara huyo amesema idara ya polisi inafaa kuwahakikishia wakenya kuwa visa hivyo havitashuhudiwa tena nchini na pia wanawake hawatapata mateso tena.
Aidha raila amesema ni jukumu la idara ya mahakama kuhakikisha wakenya wamepata haki kwa kuwachukulia hatia kali wale wote wanaojihusisha na visa hivyo vya utekaji nyara
By News Desk