HabariSiasa

Kinara wa ODM atoa wito kwa idara ya usalama na mahakama kumaliza kesi za visa vya watoto kupotea……….

Kinara wa chama cha ODM  Raila Odinga ametoa wito kwa  maasifa wa polisi  pamoja na idara ya Mahakama  kumaliza kwa haraka kesi za visa vya watu  hasa watoto na wanawakekupotea na mwishoe kupatikana wameuwawa  mara kwa mara.

Raila amesema watoto na wanawake wengi  wamepoteza maisha yao kwenye mikono ya watu ambao wanafaa kuwalinda.

Hata hivyo kinara huyo amesema idara ya polisi inafaa kuwahakikishia wakenya kuwa visa hivyo havitashuhudiwa tena nchini na pia wanawake hawatapata mateso tena.

Aidha raila amesema ni jukumu la idara ya mahakama  kuhakikisha wakenya wamepata haki kwa kuwachukulia hatia kali wale wote wanaojihusisha na visa hivyo vya utekaji nyara

 

By News Desk