HabariNewsSiasa

MIKOKOTENI HAIWEZI KUMALIZA UFUKARA RAILA AMKASHIFU RUTO…

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amemkashifu Naibu Rais William Ruto akisema kiongozi huyo amekosa sera za kubadilisha maisha ya wakenya akidai mikokoteni haiwezi kumaliza ufukara miongoni mwa jamii za wakenya.

Akizungumza huko Dabaso, kaunti ya Kilifi Raila amemtaja Ruto kama kiongozi ambaye amekosa kuwafanyia kazi wakenya anaowataja kuwa katika daraja la chini wakati akiwa naibu rais.

Kiongozi huyo aidha ameongeza kuwa Ruto ameendelea kuwahadaa wakenya kwa kutumia fedha za ufisadi wakati akiendeleza siasa zake za mikokoteni.

Kiongozi huyo ameshikilia kuwa bado mchakato wa BBI utaendelea kwa kasi na tayari wamepata mbinu za kupitisha mchakato huo licha ya kuzuiliwa na mahakama.

Raila amesisitiza ni kupitia mchakato huo ambapo fedha nyingi zitafika mashinani na kuwasaidia wakenya kupata miradi ya maendeleo.

BY REPORTER