HabariSiasa

EACC IMEKANA MADAI YA KUCHELEWESHA UCHUNGUZI WA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI ELFU 43.

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC imekana madai kuwa imechelewesha uchunguzi wa zaidi ya shilingi milioni 43 ambazo zilipotea katika kauti ya kilifi mnamo mwaka wa 2016.Akizungumza mapema hii leo afisaa mkuu katika tume hiyo Twalib Mbarak amesisitiza kuwa jinsi vyombo vya habari vilivyo toa taarifa hiyo ilikuwa makosa.Mbarak amesema kuwa tume ya EACC inalojukumu kisheria la kupambana na ufisadi, na jukumu hilo halifai kudhaniwa kwamba linaingilia kazi za serikali ya kaunti ya Kilifi katika kuhakikisha fedha hizo zilizoibiwa zinarudishwa kwenye kaunti hiyo.Aidha kulingana na gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi ambaye alikuwa mbele ya kamati ya uhasibu na uwekezaji katika bunge la seneti EACC ilitekeleza jukumu lake kikamilifu katika  kuhakisha fedha hizo zimeregeshwa kutoka kwa kampuni ambazo zilipanga njama ya kuiba pesa hizo.

 

BY GLADYS MARURA