Shule za upili kote nchini zinaendelea kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza katika muhula wa kwanza kulingana na kalenda mpya ya masomo ilivyoratibiwa na wizara ya elimu nchini.
Agnes Mulinge ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya Star of the Sea mjini Mombasa amesema kuwa shule hiyo imejiandaa vyema kuwapokea wanafunzi 465 ambao wataanza masomo wakati wowote kuanzia siku ya Jumanne.
Aidha wazazi ambao wamewapeleka wana wao katika shule hiyo wamefurahishwa na vile shughuli hiyo ya mapokezi inavyokwenda .
Jumla ya wanafunzi milioni moja wanatarajiwa kujiunga na shule za upili kote nchini kuanzia hii leo,huku kukiwa na mvutano kuhusu ufadhili wa masomo yaani bursary hususan kwa wanafunzi kutoka familia maskini.
Matumaini ya wazazi hao yako mikononi mwa wabunge wanaoendesha hazina ya ustawishaji wa maeneo bunge CDF pamoja na ufadhil wa serikali za kaunti huku serikali ya kitaifa ikiwa tayari imewafaa wanafunzi elfu 90 chini ya mpango wa elimu Scholarship.