HabariSiasa

Hakuna mtu atakaye tushurutisha kuihama Jubilee asema Naibu wa Rais William Ruto……………

Naibu wa rais William Ruto sasa anasema kuwa hakuna yeyote ambaye atawashurutisha kukihama chama cha Jubilee na kujiunga rasmi na chama cha UDA.

Akizungumza wakati wa mkutanona wabunge wa UDA nyumbani kwake Karen jijini Nairobi,Ruto amesisitiza kuwa wao sio wageni ndani ya Jubilee kwani ndio waanzilishi na watakihama kwa wakati ambao ni mwafaka kwao.

wakti huuohuo Ruto amesema uwa wako tayari kuungana na muungano wowote nchini ili kuunda muungano walio na ajenda sawa na zao za kuenua maisha ya mwananchi wa kawaida.

Aidha amesema kwamba baadhi ya viongozi wamekosoa mfumo wake wa kiuchumi maarufu ‘Bottom Up’ akiongeza kwamba ni jambo wanalolichukulia kwa uzuri ili kuboresha mfumo wake.

Hata hivyo amedokeza kwamba mfumo wake unalenga kuona kwamba tatizo la madeni linashughulikiwa kwani ni jambo ambalo linageuka donda sugu nchini

 

By News Desk