HabariKimataifaWorld

Kenya yaungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya vijana duniani…………..

Huku Kenya ikiungana na ulimwengu mzima hii leo kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana, vijana hapa Mombasa wamelalamikia kutosaidiwa na serikali katika kujikuza na kujiunua kibishara.

Vijana hao wakiongozwa na Vincent Ouma wanasema hawapewi nafasi ya kutoa hoja zao kuhusiana na changamoto ambazo vijana wanapitia kila siku kama vile suala la ukosefu wa ajira.

Naye mmoja wa viongozi wa vijana hapa Mombasa Aisha Mahamed amesema hii wiki imetengwa rasmi kote duniani ili vijana waweze kujadili jinsi wanavyoweza kutumia ubunifu kubadilisha mifumo ya chakula pamoja na kujiinua kimaisha hasa wakati huu ambapo kuna ugumu wa janga la corona.

Wawili hao wameisihi serikali ya kaunti ya Mombasa kutatua changomoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kutoa mikakati na mipango maalum ya kuwainua.

kauli mbiu ya sherehe za mwaka huu kubadilisha mifumo ya chakula, ubunifu wa vijana pamoja na afya duniani.

Hapa Mombasa sherehe hizi zinaadhimishwa katika eneo la Shanzu.

 

BY CAROLINE NYAKIO