AfyaHabari

Wananchi wahimizwa kutembelea vituo vya afya wanapoona dalili za Dengue…..

Wito umetolewa kwa wakaazi katika kaunti ya Mombasa haswa katika eneo bunge la Mvita kuhakikisha wanatembelea vituo vya afya punde tu wanapoona dalili za degue badala la kukimbia katika maduka ya kununua dawa na kujitibu.

Kulingana na Fatuma Arono afisaa wa afya katika mvita Sub-county mara nyingi wananchi hukimbilia maduka ya kununua dawa badala ya kutembelea vituo vya afya jambo ambalo analitaja kuwa hatari.

Hata hivyo Arono amewataka wakaazi wa eneo la pwani kuhakikisha kuwa mazingira yao safi ili kupigana na janga la maradhi haya hatari na kuongeza kuwa kuna maafisa wengi nyanjani ambao wanahakikisha wananchi wamepata elimu ya kutosha kuhusiana na umuhimu wa kueka mazingira kuwa safi.

Aidha kulingana na afisaa huyo kufikia sasa hali inaonekana kuwa na afueni ikilinganishwa na miezi iliyopita ambapo idadi ya maambukizi ilikuwa juu hasa katika mwezi wa 4.

 

BY GLADYS MARURA