AfyaHabari

Watu 1,437 waambukizwa corona, huku 29 wakifariki…..

Watu 1,437 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona baada  ya sampuli 10,764 kufanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita na kufanya idadi ya maambukizi kufikia 218,713.

Kati ya idadi hiyo , watu 1,377 ni wakenya huku 60 wakiwa ni raia wa kigeni,738 ni wanaume na 699 wakiwa ni wanawake mdogo zaidi ni mtoto wa miezi 2 na mzee zaidi ana miaka 100.

Hata hivyo wagonjwa 29 wamethibitishwa kuaga dunia kutokana na makali ya korona na kufanya idadi ya walioangamia kutokana na janga hili kufikia 4,302.

Aidha wagonjwa 1,056 wamepona maradhi hayo 963 kutoka katika utuzaji wa nyumbani na 93 kutoka katika vituo vya afya mbalimbali nchini na kufanya idadi ya waliopona virusi hivyo kufikia 201,054.

Kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa vipya  496,Nakuru 139,Mombasa 100,Taita Tateta 28,Kilifi 28,Lamu 17,Kwale 1 miongoni mwa kaunti zengine.

By Gladys Marura