AfyaHabariNews

Kenya kupokea dozi nyingine za Astrazeneca leo usiku…..

Waziri wa afya Mutahi Kagwe leo usiku anatarajiwa kupokea dozi elfu 400 za chanjo ya Astrazeneca kutoka nchini Uingereza.

Chanjo hiyo ni ya awamu ya pili ya chanjo elfu 800 zilizotolewa na Uingereza kufuatia makubaliano wakati wa ziara ya rais Uhuru Kenyatta nchini humo mwezi uliopita.

Wiki mbili zilizopita Kenya ilipokea dozi nyingine elfu 180 za chanjo ya Astrazeneca kutoka taifa la Ugiriki.

Kufikia sasa watu milioni 2, elfu 53 mia 717 wamechanjwa miongoni mwao milioni 1, elfu 305 mia 850 wamepokea dozi ya kwanza huku efu 747 , 867 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

By Warda Ahmed