AfyaHabariKimataifa

Serikali yatakiwa kuchukua jukumu la kuhakikisha walimu wote wamechanjwa……

Serikali kupitia wizara ya afya imetakiwa kuchukuwa jukumu la kuhakikisha kuwa walimu wote wamechanjwa kwa kuwafuata walimu katika shule zote nchini.

Kulingana na Brown Safari mmiliki wa shule ya kibinafsi na vilevile muaniaji wa  kiti cha uwakilishaji wadi katika wadi Mtepeni kaunti ya kilifi,  serikali inatakiwa kuzunguka shule baada ya shule ili kuwapa walimu chanjo dhidi ya korona kwani jukumu la mwalimu ni kufundisha akiongeza kwamba zoezi hilo la kuzunguka kutafuta chanjo ni gharama kwa walimu hasa wa kibinafsi.

Aidha Safari ameitaka serikali kuingilia kati na kusaidia kufunguliwa kwa shule za kibinafsi ambazo zilifungwa baada ya janga la korona kuingia nchini kwani kufikia sasa bado kuna shule ambazo hazijafunguliwa na watu wengi wamepoteza ajira kupitia kufungwa kwa shule hizo.

Haya yanajiri huku walimu wakiwa na siku tano tuu kuhakikisha kuwa wamechanjwa dhidi ya virusi vya korona ili kudhibithi msambao wa maradhi hayo.

BY DAVID OTIENO.