HabariNews

Asilimia 80 ya shule za chekechea kilifi zajengwa kuimarisha elimu……

Zaidi ya asilimia 80 ya shule za chekechea kaunti ya Kilifi tayari zimejengwa na serikali ya kaunti hiyo ili kukimu idadi ya wanafunzi eneo hilo.

Kulingana na waziri wa ugatuzi Profesa Gabriel Katana hatua hiyo inalenga kuimarisha sekta ya elimu katika miaka ijayo.

Profesa Katana anasema mbali na majengo ya shule hizo serikali imeajiri waalimu pamoja na kununua vitabu kwa wanafunzi wa chekechea akiongeza kuwa makundi ya akina mama pia yamepewa kipaumbele.

Wakati uohuo Katana anasema zaidi ya asilimia 90 ya barabara nyanjani zimefunguliwa na kurahisiashia wakulima kusafirisha mazao yao.

Amesema ujio wa serikali za ugatuzi umesababisha miradi mbali mbali kusambazwa nyanjani hivyo kuimarisha maisha ya wenyeji.

Waziri huyo ameyasema haya siku chache tu kabla kuandaliwa kongamano la ugatuzi katika kaunti ya Makueni.

By Malindi correspondent