HabariNewsSiasa

ODM kufanya mkutano huko Sikri eneo la Nyanza……..

Chama cha ODM kinatarajiwa kufanya mkutano katika eneo la Sikri huko Nyanza.

Mkutano huo ambao utaongozwa na kinara wa chama hicho Raila Odinga na utawaleta pamoja viongozi mbalimbali ikiwemo wabunge na masenata huku watu 700 wakiruhusiwa kuhudhuria.

Kamishna wa Nyanza Magu Mutindika amewataka viongozi na wananchi watakaohudhuria mkutano huo kutilia maanani masharti yaliyowekwa na wizara ya afya pamoja na kudumisha amani akisema hatataka kuzuke makabiliano baina yao na maafisa wa polisi.

Hata hivyo Mutindika amewataka makamishana wote wa idara husika kuhakikisha kuanzia kesho mikutano yote inayofanyika eneo hilo inazingatia masharti ya kudhibiti msambao wa virusi vya Corona.

Aidha amewasihi viongozi kusitisha mikutano ya hadhara.

BY Joyce Kelly