Naib wa rais William Ruto ameisifia idara ya mahakama kwa juhudi zake za kuhakikisha kwamba katiba ya Kenya inazingatiwa.
Akizungumza nyumbani kwake eneo la Karen jijini Nairobi Ruto amepongeza ujasiri wa jopo la majaji saba waliotoa uamuzi wa kutupilia mbali mapendekezo ya kufanyia katiba marekebisho wakiongozwa na rais wa mahakama ya rufaa jaji Daniel Musinga
Ruto amewataka viongozi kusonga mbele akiwasihi kuwafanyia wakenya kazi kwa kuangazia maslahi yao hususan uchumi na kuanzisha nafasi za ajira kwa kila mmoja ili kukuza na kuendeleza uchumi wa kenya.
Vile vile amesema kuwa watajenga ushirikiano na vijana katika juhudi za kuimarisha uchumi wa nchi, huku akiwaomba vijana kukataa kudhulumiwa na kujitokeza katika uundaji wa serikali mpya.
BY JOYCE KELLY