HabariNewsSiasa

WAKAAZI TANA RIVER KUTOKUBALI KUGAWANYWA KWA MISINGI YA UKABILA, DINI NA MIRENGO YA KISIASA

Mwenyekiti wa baraza la muungano wa kidini kaunti ya Tana River Rev, Shadrack Mukolwe amewataka wakaazi wa kaunti ya Tana River kutokubali kugawanywa kwa misingi ya ukabila, dini na mirengo ya kisiasa huku uchaguzi mkuu mwaka ujao ukikaribia.

Aidha Mkolwe amewasisitizia vijana wasitumiwe vibaya na wasisiasa kuzua vurugu kwenye azma yao ya kisiasa badala yake wajishughulishe na ujenzi wa taifa.

Vile vile awaomba wakazi wa Tana River kutojihusisha sana na siasa za kitaifa badala yake kujenga msingi bora ya siasa za kaunti hiyo ili amani kuendelea kudumu.

BY NEWS DESK