Waziri wa masuala ya usalama wa ndani dkt Fred Matiangi amefika mbele ya kamati ya utawala ya bunge la kitaifa kuhojiwa kuhusu suala la usalama wa naibu rais William Ruto.
Matiangi ameanza na kuzungumzia na idadi ya maafisa ambao wanawalinda viongozi mbali mbali nchini akisema kwamba kuna maafisa elfu 4 wa polisi wanaowalinda maafisa mbali mbali wa serikali kote nchini, na naibu wa rais William Ruto ana maafisa 74 wanaomlinda na kulinda na makaazi yake pamoja na shughuli zake mbali.
Amesema hata dereva wa naibu wa rais ni afisaa wa GSU huku wale wa utawala walipewa jukumu la kulinda nyumba za Ruto akisema maafisa wa GSU waliondolewa walikuwa wakilinda nyumba za Ruto za Sugoi na Karen.
Amesema kwa sasa maafisa wa kitengo cha ulinzi cha rais wanaendelea kumlinda Ruto.
BY NEWS DESK.