HabariNews

Maafisa wa DCI Malindi wachunguza kisa baada ya mtoto wa miaka 7 kupigwa shoti huko Takaye…….

Maafisa wa uchunguzi wa jinai mjini Malindi wanachunguza kisa ambapo mtoto wa umri wa miaka Saba aliaga dunia baada ya kupigwa shoti ya nyaya za stima kule Takaye viungani mwa mji huo.

Kulingana na kamanda wa polisi mjini Malindi John Kemboi marehemu alikuwa akicheza karibu na duka na wenzake kabla ya tukio hilo kutokea.

Kemboi anasema maafisa wake wanachunguza endapo kebo hiyo ya stima ilikuwa wazi hivyo kupelekea maafa hayo ama watoto hao waliifungua.

Hata hivyo babake marehemu Francis Mangi ametilia shaka jinsi kebo hiyo ya umeme iliwekwa kwenye nyumba hiyo akidai huenda haikuwekwa kama ilivyostahili.

BY NEWS DESK