Wasichana watano kati ya makumi ya wanafunzi waliotekwa nyara kutoka shule moja ya upili katika jimbo la Zamfara kaskazini mwa Nigeria wametoroka kutoka kwawatekaji nyara wao.
Watu waliojihami kwa bunduki walishambulia shule yao katika mji wa Kaya-Maradun Jumatano na kuwateka zaidi ya wanafunzi 70 – wengi wao wakiwa wasichana – na mfanyikazi mmoja mwandamizi.
Wazazi wa wanafunzi hao waliiambia BBC kwamba watoto hao waliweza kutoroka wakati watu hao waliojihami walipokuwa wakiwagawanya katika vikundi kwa harakati zaidi kuelekea msituni. Walirejea nyumbani usiku sana.
Polisi wa Zamfara walithibitisha tukio hilo lakini walisema kwamba wasichana wa shule “waliokolewa” bila kutoa maelezo.
Vikosi vya usalama vinasema wanajaribu kupata makumi ya wanafunzi wengine ambao bado wameshikwa mateka.
BY NEWS DESK.