HabariKimataifaNews

Kundi la Taliban linatazamiwa kutangaza serikali ndani ya siku zijazo…

Kundi la Taliban linatazamiwa kutangaza serikali ndani ya siku zijazo licha ya mapigano makali yanayoendelea katika bonde la Panjshir, ambako vikosi vinavyopambana na wapiganaji wa Kiislamu walio na misimamo mikali, vimedai kukabiliwa na mashambulizi mazito.

Hapo jana kulisikika milio ya risasi mjini Kabul, kusherehekea ushindi kufuatia uvumi kwamba bonde la Panjshir limeangukia mikononi mwa Taliban, lakini Wataliban hawakutoa taarifa yoyote rasmi.

Wapiganaji kutoka National Resistance Front, kundi linaloundwa na wanamgambo wanaoipinga Taliban na vikosi vya zamani vya usalama vya Afghanistan , wanaaminika kuwa na akiba kubwa ya silaha katika.

BY NEWS DESK