Uncategorized

GAVANA WA MOMBASA ASSISITIZA KUWA BBI ILILENGA KUIMARISHA YA WAKENYA…………….

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho amesisitiza kuwa BBI ililenga kuwaunganisha wakenya vilevile kuimarisha mazingira ya wananchi ya kufanyia kazi.

Kulingana na Joho siasa zimechangia pakubwa katika kuangushwa kwa mchakato huo wa BBI  kwenye mahakama za rufaa na mahakama kuu na kusema kuwa kuangushwa kwa BBI kumekuwa pigo kubwa sio kwake tu ila pia kwa kinara wa ODM Raila Odiga vilevile rais Uhuru Kenyatta.

Hata hivyo gavana Joho anasema pendekezo la kuongeza mgao wa fedha katika kaunti kutoka asilimia 15 hadi 35 sasa itasalia kuwa ndoto iwapo BBI haitanusuriwa.

Haya yanajiri huku mahakama ya juu inasubiriwa kutoa uamuzi wa iwapo BBI itaendelea au la.

Aidha tume ya uchaguzi  na mipaka nchini IEBC imeifahamisha mahakama hiyo itakata rufaa kufwatia uamuzi kuwa hawakuwa na makamishna wa kutosha wakati wa kuhesabu saini za BBI na hata kuwasilisha mswaada kenye mabunge ya kaunti.

 

By News Desk