AfyaHabariKimataifaNews

DRC Yapokea dozi 250,000 za chanjo ya Moderna….

Jamhuri ya kidemokrasia yaCongo imepokea dozi 250,000 za chanjo ya Corona aina ya Moderna.

Ni mara ya kwanza DRC kupokea chanjo nyingine isioyokuwa ya AstraZeneca.

Rais wa DRC, Felix Tshisekedi mwenyewe alisita kuchukua chanjo ya AZ na kuahidi kupewa chanjo tofauti wakati zitakapopatikana nchini.

Kundi hili la kwanza la dozi 250,000 za chanjo ya Moderna ni sehemu ya chanjo milioni sita tofauti ambazo Nchi hiyo ya Afrika ya Kati imekuwa ikingojea tangu, Julai.

DRC ni moja ya nchi ambazo kuna pingamizi ya juu kupokea chanjo ya Corona barani Afrika.

Tangu kuzinduliwa kwa kampeni ya chanjo dhidi ya covid-19, mnamo Aprili 19, 2021, chini ya watu laki moja wamepokea chanjo hizo. Zaidi ya dozi elfu 300 za AZ zililazimika kuharibiwa wakati zilipomalizika muda wa matumizi Juni na Julai iliyopita.

BY NEWS DESK