HabariMazingiraNews

Ndovu saba wazua taharuki huko Rabai kaunti ya Kilifi…..

Maafisa wa polisi wametumwa kushika doria katika vijiji mbali mbali eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi ili kuhakikisha kwamba ndovu saba waliovamia kata ya ruruma leo asubuhi hawajashambulia binadamu.

Kamanda wa polisi wa Rabai Fred Abuga anasema tayari amewasilisha taarifa kwa shirika la huduma kwa wanyamapori KWS ili kuchukuwa hatua kuhusu wanyama hao.

Anasema kufikia sasa hakuna mtu yeyote ambaye ameshambuliwa.

Inakisiwa kwamba huenda ndovu hao wametoka mbuga ya Tsavo Mashariki baada ya kuhangaika kutafuta maji na malisho.

Ndovu hao wameingia katika shule za upili eneo hilo na kutatiza shughuli za masomo huku hali ya taharuki ikiendelea kushuhudiwa katika vijiji mbali mbali vya Rabai.

BY NEWS DESK