Habari

Matiangi awaonya wanasiasa wanaoshirikiana na majambazi Laikipia………

Waziri wa usalama wa ndani nchini Dkt Fred Matiangi amewaonya wanasiasa ambao wanashirikiana na majambazi wanaoendeleza uvamizi huko kaunti ya Laikipia.

Akiongea huko Ol Moran, Matiangi amesema watahakikisha uvamizi huo unakomeshwa mara moja ili kuepusha maafa zaidi.

Amesema wanasiasa wanaoendeleza mikutano eneo hilo kwa lengo la kuwahangaisha wananchi watakamatwa.

Amesema makamanda wa polisi sasa watakuwa wakiendeleza mafunzo yao eneo hilo ili kukabiliana na wavamizi hao.

Matiangi ametangaza kuunganishwa kwa maeneo ya Ol- Moran, Sipili na Ol-Ng’arua huko Laikipia na kujumuishwa kuwa wilaya moja iliyopewa jina la KIrima ili kuimarisha usalama eneo hilo.

 

By Warda Ahmed