HabariNews

Jamaa wawili wanaoshukiwa kumbaka mwanamke mwenye akili tahira wakamatwa huko Lamu…..

Idara ya upelelezi wa jinai DCI imefanikiwa kuwakamata watu wawili wanaoshukiwa kumbaka mwanamke mwenye akili taahira  katika kaunti ya Lamu.

Wawili hao Shadrack Murimi Maina mwenye umri wa miaka 45 na Hiribae Kokame mwenye umri wa miaka 43 walijidai kuwa wasamaria wema kisha kumtendea unyama huo ndani ya nyumba moja katika eneo la sinambio.

Wawili hao ambao walikuwa wameandamana na mzee wa Nyumba kumi Samuel Ngumi walikuwa wakishika doria walipokutana na mwanamke huyo akipika chai kwenye eneo la tukio.

BY NEWS DESK