HabariKimataifaNews

Korea kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa marefu, yasema Korea Kusini…

Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa marefu kutoka pwani ya mashariki ya taifa hilo, jeshi la Korea Kusini limethibitisha.

Japan pia iliripoti kwamba kuna kitu kilichofyatuliwa kuelekea angani ambacho inahisi huenda ni kombora la masafa mrefu.

Waziri mkuu wa Japan Yoshihide Suga amelitaja jaribio hilo la kombora kama la kikatili akisema linatishia usalama na amani ya eneo hilo.

Ni jaribio la pili la silaha kufanywa wiki hii, huku la kwanza likiwa kombora la masafa mafupi.

Haijulikani ni wapi makombora hayo yalianguka , lakini mkuu mwenza wa majeshi nchini Korea kusini amesema kwamba jeshi la taifa hilo limejiandaa vilivyo likishirikiana kwa karibu na lile la Marekani.

BY NEWS DESK