HabariNews

Taharuki imetanda katika kijiji cha Wasaa kaunti ya Kwale kutokana na uwepo wa nyati ambaye anawahangaisha.

Wakazi wa Kikoneni wanasema kwamba shughuli za ukulima ebneo hilo limeathirika pakubwa kwa sababu mara nyingi wanapolima na mahindi kuwa nyati huyafanya kitoweo mazao yao ya shambani.

Aidha Mwanamume mmoja amevamiwa na kuvunjwa mguu na Nyati wakti akiwa malishoni.

Haya yanajiri licha ya serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium pamoja na idara ya wanyama kuendesa zaoezi ya kuwahamisha Nyati na ambapo walihamisha nyati tisa na kuwapeleka katika mbuga ya wanyamapori ya Tsavo kaunti ya Taita Taveta mwaka jana.

BY JOYCE MWENDWA