HabariNews

Idadi kubwa ya waendesha Boda Boda mjini Malindi wanakosa vibali…

Imebainika kuwa idadi kubwa ya waendesha Boda Boda mjini Malindi wanakosa vibali muhimu katika utenda kazi wao.

Kulingana na taarifa kutoka kwa idara ya polisi eneo hilo waendesha Boda Boda 7 kati ya kumi hawana vibali wala pikipiki zao zinakosa stakabadhi za utendakazi.

Kulingana na kamanda wa polisi eneo hilo John Kemboi hatua hiyo inachochewa na hatua ya mamia ya vijana kukosa ajira maalum hivyo kusababisha vijana hao kuingia katika sekta hiyo.

Kemboi anasema wengi wa vijana hao ni wale waliomaliza masomo Yao ya kidado Cha nne huku wengine wakikosa kujiunga na shule za upili kutokana na changamoto za maisha.

Hata hivyo kamanda huyo amewashauri vijana hao kujiunga na vyuo vinavyotoa mafunzo ya uendeshaji pikipiki Ili wapate vibali vya kufanya kazi hiyo.

Kemboi amesema sekta hiyo imetoa ajira kwa maelfu ya vijana eneo hilo na endapo wataendelea kufanya kazi bila vibali huenda idadi ya ajali ikaongezeka mara dufu.

Amesema maafisa wake wataanzisha msako mkali katika siku za usoni ili kuwanasa madereva wote watakao kosa vibali eneo hilo.

BY NEWS DESK