AfyaHabariMombasaNews

Wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya makadara wanazidi kuililia serikali ya kaunti ya Mombasa…

Wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya makadara wanazidi kuililia serikali ya kaunti ya Mombasa kuhusiana na mgomo wa wauguzi pamoja na madaktari unaoendelea.

Kulingana na baadhi ya wagonjwa waliozungumza na meza yetu ya habari ni kuwa kwa sasa wanateseka kwani wengine wao wametoka katika maeneo ya mbali ili kufika hospitalini humo kuwaona madaktari kulungana na walivyo agiziwa.

Wagonjwa hao kwa sasa wanaitaka serikali ya kaunti hii kuingilia kati na kutatua swala hilo na pia kutafuta suluhu la kudumu ili waweze kuzuia migomo ya mara kwa mara katika kaunti.

Haya yanajiri baada ya madaktari katika kaunti hii kujiunga na wahudumu wa afya katika mgomo ambao unaendelea kushuhudiwa.

Kauli hizi zinajiri huku mgomo wa madaktari kushinikiza kulipwa mishahara yao, bima ya NHIF pamoja na kulipwa marupurupu yao ukiingia siku yake ya pili hii leo baada ya mazungumzo kati ya muungano huo na naibu gavana wa kaunti ya Mombasa William Kingi kugonga mwamba.

Kulingana na katibu wa muungano Shaban Nassir ameidokezea sauti ya pwani kwamba hadi kufikia sasa serikali ya kaunti ya Mombasa imeshindwa kushughulikia matakwa yao.

Ni kauli ilioungwa mkono na mwenyekiti wa muungano wa madaktari Hassan Ahmed anayesema watawafungulia mashtaka wale wote waliohusika na kukosekana mishahara kwa madaktari hao pamoja na marupurupu yao.

BY NEWS DESK