HabariMombasaNewsSiasa

BAADHI YA VIONGOZI WA PWANI WASHIKILIA MSIMAMO WA KUSIMAMA NA RAILA ODINGA KWENYE UCHAGUZI MKUU UJAO WA 2022.

Mbunge wa likoni Mishi Mboko amemkashifu vikali naibu wa rais William Ruto akidai kuwa Ruto amekuwa mwenye kupinga kila maendeleo humu nchini.

Akizungumza hapa mombasa mbunge huyo amesema kuwa kama kweli Ruto angekuwa na maono ya kuendeleza uchumi pamoja na usawa wa jinsia basi hangekuwa katika mstari wa mbele kupinga juhudi za kubadilisha katiba ili kuzidi kuleta rasilimali mashinani.

Kiongozi huyo ameendelea kukashifu vikali mfumo wa bottoms up akidai kuwa ni wa kuregesha nyuma wakenya kwani kufikia sasa idadi kubwa ya vijana wameenda shule hivyo basi wanapaswa kupea ajira ifaao.

Amesema haya katika kongomano lilowaleta pamoja viongozi wa chama cha ODM katika kaunti ndogo ya Nyali kwenye ziara ya  azimio la umoja ukiongozwa na kiongozi wa chama cha ODM raila odinga .

Huku hayo yakijiri baadhi ya wajumbe waliokongamana katika mkutano huo wameahidi kuungana kumtawaza Raila Odinga kuwa Rais wa tano wa taifa  .

Wakiongozwa na mjumbe kutoka kaunti ndogoi ya Likoni Musa Mwanda  wamesema lengo lao kuu ni kuimarisha  ushikamano wa chama hicho

Aidha kulingana na katibu mkuuu wa chama hicho Edwin Sifuna  chama cha ODM kiko imara hivyo fununu zinazodai kuwa chama hicho kinayumba sio za ukweli.

BY DAVID OTIENO