HabariNews

Idadi ya vifo kutokana na ajali za barabarani yaongezeka…

Idadi ya vifo kutokana na ajali za barabarani mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na kipindi sawia na hiki mwaka jana.

Kulingana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Usafiri na Usalama wa Taifa (NTSA) umebaini kuwa kumekuwa na ongezeko la asilimia 25 ya ajali za barabarani kufikia Septemba 20, 2021.

Uendeshaji wa gari kwa kasi, kuyapita magari mengine kiholela, kati ya masuala mengine yamehusishwa na ongezeko la ajali hizo.

Kati ya Januari 2021 na Septemba 20, 2021, watu 3,212 wamehusika katika ajali ikilinganishwa na watu 2,560 waliofariki mwaka jana, hii  ikiwa ni ongezeko la watu 652.

Kati ya wale walioaga dunia mwaka huu, watu 1,111 ni wale waliokuwa wanatembea kwa miguu, madereva 311, abiria 520, abiria 318 wa kidonge, wapanda baisikeli 61 na waendesha pikipiki 891.

BY NICKY WAITA