AfyaHabariNews

Serikali ya kaunti ya Kwale inatarajia kupokea chanjo ya tatu ya virusi vya corona ya aina ya Johnson & Johnson.

Gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema kuwa chanjo hiyo inayotarajiwa hivi karibuni inalenga kuimarisha juhudi za serikali za kuwachanja wananchi.

Mvurya amesema kuwa kwa sasa wanaendelea kutoa chanjo ya AstraZeneca na Moderna kwa wakaazi wa kaunti hiyo.

Gavana huyo aidha ameelezea kuridhishwa kwake na idadi ya watu inayojitokeza kupokea chanjo hizo.

Mvurya amewataka wakaazi kuchukua tahadhari ya kujilinda dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Zaidi ya wakaazi elfu 16 wamepokea chanjo ya corona katika ya Kwale.

BY NEWS DESK