AfyaHabariNews

Idadi kubwa ya wakaazi kaunti ya Kilifi wajihusisha na upangaji uzazi

Imebainika kuwa idadi kubwa ya wakaazi kaunti ya Kilifi wanajihusisha na upangaji uzazi kama njia mojawapo ya kuimarisha maisha ya vizazi vijavyo.

Kulingana na mshirikishi wa mpango huo kaunti ya Kilifi Ken Miriti kwasasa idadi kubwa wanaume wanatumia njia mbali mbali za kupanga uzazi kinyume na awali.

Miriti anasema zaidi ya asilimia hamsini imeongezeka kutoka kwa asilimia ya awali ya 30.

Kauli yake imeungwa mkono na Priscar Deche anayesema kwasasa idadi ya mimba za mapema kwa wanafunzi wa shule imepungua kwa kiasi kikubwa akisema ni ushahidi kuwa mpango huo unazingatiwa.

Amesema zaidi ya asilimia 40 ya wasichana kaunti hiyo kwa sasa wanatumia njia mbali mbali za kupanga uzazi hivyo kupunguza visa vya mimba za mapema.

BY NEWS DESK