HabariNewsSiasa

UTAWALA WA JUBILEE WAONYWA DHIDI YA UTUMIZI MBAYA WA FEDHA ZA UMMA.

Sawa na kifaranga anaye onywa dhidi ya ku randa randa kwenye misitu, Utawala Jubilee kwa mara nyengine umeonywa dhidi ya utumizi mbaya wa fedha za Umma kwani Taifa linaelekea pabaya kutokana na madeni kila kipembe.

Muhasibu Mkuu wa Serikali Nancy Gathungu ameonya kwamba bajeti iliyopendekezwa na Wizara ya Fedha na kuidhinishwa na Bunge Mwezi Juni mwaka huu inapaswa kutathminiwa upya iwapo Kenya ina nia ya kujikwamua kutoka kwa madeni.

Aidha muhasibu huyo ambaye alifika mbele ya Bunge la Seneti ya Fedha na Bajeti, ameitaka Serikali kudhibiti gharama zake akisema kwamba mapato au ushuru unaokusanywa na Serikali kamwehautoshelezi bajeti ya Kenya ambayo ni zaidi ya Trilioni 3.

Ikumbukwe kwamba kwa sasa Deni limefikia asilimia 84 ambayo ni sawia na shilingi Trilioni 9 zilzoafikiwa kuwa kilele cha deni la Taifa baada ya suala hilo kuidhinishwa na Bunge miaka miwili iliyopita.

Wakati uo huo Ufisadi, Ahadi Tasa, ubinafsi, Usimamizi mbovu wa Fedha, Gharama ya juu ya mishahara ya wachache Serikalini pamoja na kuzinduliwa kwa miradi zaidi, kwa pamoja kumechangia hali hii

Swali ni Je, kupunguza mishahara ya Rais na Naibu wake kwa asilimia 80 ulifanyika?

Na Je, Mawaziri walikatwa asilimia 30 ya mishahara yao jinsi Rais Uhuru Kenyatta alivyoahidi mwezi Machi Mwaka uliopita?

BY NEWS DESK