HabariNews

Bunge la kaunti ya Kilifi kujadili mswada wa uchimbaji mawe katika wadi ya Jaribuni…

Bunge la kaunti ya Kilifi, linalenga kujadili mswada wa kuifanyia marekebisho sheria ya uchimbaji mawe katika wadi ya Jaribuni eneo bunge la Ganze.

Kuingana na mwakilishi wa wadi ya Jaribuni Maitha Masha, sheria inayotumika kwa sasa ni ya uchimbaji madini na wala sio mawe.

Masha aliyewasilisha mswaada huo bungeni, amesema sheria hiyo inalenga kuangazia maslahi ya wananchi wa eneo hilo.

BY NEWS DESK