HabariKimataifaNews

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema kuwa serikali ya Ethiopia imewaachilia huru madereva wa misaada walio waliokamatwa wiki iliyopita.

Katika kikao mjini New York, Haq amesema kwamba madereva 34 wameachiliwa lakini wengine 36 bado wanazuiliwa.

Haq aidha alitumai kuwa wafanyikazi waliosalia wa kandarasi na wafanyikazi 10 wa kitaifa wa UN waliokamatwa na mamlaka wataachiliwa.

Kukamatwa kwao kwa wafanyikazi wa UN na wafanyikazi wa kandarasi kulifuatia tangazo la serikali ya shirikisho la hali ya hatari mapema mwezi huo.

Hatua hiyo ilichukuliwa wakati wapiganaji waasi wa Tigray walitishia kuingia mji mkuu wa Addis Ababa.

Haya yanajiri huku maelfu ya watu wakiuawa na wengine kuyahama makazi yao katika vita vya mwaka mzima kati ya mamlaka ya Ethiopia na wapiganaji waasi wa Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

BY NEWS DESK