HabariNews

Wazee wa Kaya kaunti ya Kilifi watoa wito kwa viongozi eneo hilo kukarabati alipozikwa shujaa Mekatilili wa Menza.

Wazee wa Kaya kule Magarini kaunti ya Kilifi wametoa wito kwa viongozi eneo hilo kukarabati mahali alipozikwa shujaa wa mijikenda Mekatilili wa Menza.

Wakiongozwa na Charo Maitha Wazee hao wanasema kupitia kwa njia hiyo utamaduni wa jamii hiyo utadumishwa.

Wanasema kwa muda sasa eneo alipozikwa shujaa huyo limetelekezwa huku jamii yake ikiachwa ikihangaika licha ya shujaa huyo kupigania uhuru wa taifa.

Wakati uohuo wazee hao wameisuta serikali ya kaunti hiyo kwa kutotilia maanani na kuimarisha utamaduni wa jamii hiyo.

Wanasema kwa sasa wameamua kurekebisha mahali alipozikwa shujaa huyo wakisema huenda masaibu wanayopitia yanatokana na shujaa huyo kukosa amani kutokana na kutotambuliwa.

Shujaa Mekatilili alihusika katika vita vya kwanza vya dunia na alipata umaarufu baada ya kudaiwa kumpiga kofi mbeberu kule Shakahola.

BY NEWS DESK