HabariNews

Takwimu zaonyesha takriban watu 43 wamepotea mwaka huu.

Kenya imerikodi idadi kubwa zaidi ya watu kupotea kwa njia tatanishi hii ni ya baada takwimu kuonyesha kuwa takriban watu 43 wamepotea mwaka huu.
Kulingana na shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika, wakenya hao wanaaminika kupotea mikononi mwa asasi za usalama huku wengine wakiaminika kuawa.
Kulingana na takwimu hizo Ukanda wa Pwani imerikodi idadi kubwa zaidi baada ya watu 29 kupotea kwa njia isiojulikana.
Haki Afika aidha inadai kuwa idadi hiyo imerikodiwa kati ya mwezi January hadi November mwaka huu.
Kaunti ya mombasa inaongoza na visa 17, kwale 9 Nairobi 7 Kajiado 4, Lamu 3, Kiambu na wajir zimerikodi kesi 1 mtawalia.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Khalid Hussein ametoa wito kwa wizara ya usalama nchini kupitia waziri wa wizara hiyo Dr Fred Mtiangi kuingilia kati swala hilo na kushirikiana na mashrika yanayotetea haki za kibinadamu ili kukomesha kabisa visa hivyo.

BY NEWSDESK