Rais wa Uganda Yoweri Museveni anasema kundi la waasi la Allied Democratic Forces linastahili kujisalimisha huku akisisitiza kuwa serikali yake imejitolea kukabiliana na ugaidi.
Katika hotuba iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni siku tano baada shambulio dhidi ya mji mkuu wa Kampala, Museveni amesema ADF wamejiamini sana kwa sababu wanaweza kutembea huru katika kambi za kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wanajishughulisha na uchimbaji madini na biashara za mbao.
Hata hivyo amesema kuwa Uganda itaendelea kuwasaka wanachama wa kundi hilo na kuongeza kuwa ni vyema wale ambao hawajasalimisha silaha zao wafanye hivyo.