HabariNews

Polisi waimarisha ulinzi kwa jaji wa Mahakama Kuu Anthony Mrima

Polisi wameimarisha ulinzi kwa jaji wa Mahakama Kuu Anthony Mrima kutokana na madai ya kwamba amepokea vitisho kuhusiana na maisha yake.
Haya yanajiri siku kadhaa baada Jaji Mrima kumhukumu kifungo cha miezi minne gerezani kwa mkurugenzi wa idara ya upelelezi George Kinoti.
Katika taarifa afisa mkuu wa usalama wa wafanyikazi wa idara ya mahakama Lazurus Opicho ni kwamba amemuongezea walinzi jaji Mrima katika juhudi za kukabili vitisho hivyo baada ya kuwasiliana naye kuhusu madai ya maisha yake kuwa hatarini.
Opicho aidha amemuagiza jaji Mrima kuandika taarifa rasmi katika kituo cha polisi ili kuwawezesha kuanza uchunguzi.
Kulingana na Opicho ni kwamba Jaji Mkuu Martha Koome alitoa agizp hilo baada ya kupokea taarifa hiyo kuhusu vitisho Jaji Mrima.
Vile vile, ameongeza kuwa ni muhimu kutambua kwamba usalama wa Majaji na Mahakimu wote nchini ni muhimu.
Itakumbukwa kuwa siku ya Alhamisi jaji Mrima alitoa uamuzi wa kumfunga Kinoti jela kwa miezi minne kufuatia hatua yake ya kukiuka agizo la mahakama la kumtaka kumrejeshea silaha mfanyibiashara Jimmy Wanjigi.