HabariNews

Wajumbe wa Chama cha Wiper wanatarajiwa kumuidhinisha rasmi Kinara wa Chama hicho Kalonzo Musyoka kuwania Urais.

Wajumbe hao wanakutana katika uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi huku Vinara wote wa One Kenya Alliance OKA wakitarajiwa kuhudhuria vile vile Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga.
Danson Mwashako ni Mbunge wa Wundanyi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wiper ambaye ameeleza kwamba shughuli nyengine aidha itakuwa ile ya kuzindua rasmi rangi mpya za Chama hicho.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha KANU Nick Salat amesema kwamba hatua ya kuhuduria hafla hiyo ni ishara ya Umoja na ushirikiano na kile cha Wiper, ikizingatiwa kwamba Vyama hivyo vipo katika Muungano wa OKA.
Itakumbukwa kwamba kufikia sasa Vinara wa OKA walioidhinishwa rasmi na wajumbe wa Vyama vyao kuwania Urais ni pamoja na Gideon Moi wa KANU na Moses Wetangula wa FOED KENYA huku wajumbe wa ANC wakiwa bado hawajafanya halfa rasmi ya kumuidhinisha Musalia Mudavadi.

BY NEWS DESK