HabariNewsSiasa

Mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Mombasa awaonya wagombea dhidi ya kujipiga kifua…

Mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Mombasa Mohammed Hamid amewaonya wagombea kupitia chama hicho dhidi ya kujipiga kifua na kutumia kauli ambazo huenda zikawagawanya na kusababisha mtafaruk miongoni mwa jamii.
Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho mtaa wa Ganjoni kaunti ya Mombasa baada ya kumkaribisha mgombea wa kiti cha ubunge cha Mvita Mohammed Machele, mwenyekiti huyo amesema iwapo kuna kiongozi ambaye hatafurahishwa na jambo katika chama hicho basi anatakiwa kufata utaratibu uliowekwa na chama ili kupata haki.
Aidha Mohammed amechukua fursa hiyo kuwarai wafuasi wa chama cha ODM kujisajili kuwa wanachama, akiweka wazi kuwa wanachama pekee ndio watakaoshiriki katika kura za mchujo hivyo kuwataka kufanya uamuzi wa kujiandikisha mapema ili kumuwezesha mgombea wao kuchukua tiketi iwapo atashinda kwenye mchujo.
Vilevile Muhamed amezidi kuwahakikishia wafuasi wa chama cha ODM kuwa mchujo wa chama hicho utakuwa huru na haki. Akiwataka wafuasi kuzidi kuwa na imani na uongozi wake.

BY DAVID OTIENO