Huku siasa zikipamba moto nchini na wananchi wakijiandaa kwaajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, baadhi ya viongozi wa kidini wamejitokeza kuhamasisha na kuubiri amani miongoni mwa wanasiasa na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye kipindi cha Baraza letu Sheikh Hassan Mubarak ambaye pia ni mwenyekiti wa Muungano wa Waislam wa Al-Wahdah katika Kaunti ya Kilifi amesema kwamba matukio mengi ya ukosefu wa usalama haswa wakati wa siasa yamechangiwa pakubwa na viongozi wa kisiasa kutowahusisha viongozi wa kidini katika swala zima la ushauri.
Hata hivyo amekashif tabia za baadhi ya viongozi wa kidini wanaotoa Muongozo unaonuwia kuwanufaisha wao binafsi na mwanasiasa husika huku mwananchi wa kawaida akikandamizwa.
BY MWANAISHA KAILO