AfyaHabariKimataifaNewsTravelWorld

HAKUNA MIPANGO YA KUPIGA MARUFUKU KUINGIA HUMU NCHINI KUTOKANA NA AINA MPYA YA CORONA.

Serikali haina mpango wa kupiga marufuku safari za kutoka na kuelekea Mataifa ambayo yameripoti aina mpya ya Virusi vya Corona vya Omicron.
Ndiyo kauli ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Susan Mochache ambaye amesema kwamba Wizara hiyo imeimarisha ukaguzi kwenye maeneo ya Mipakani na viwanja vya ndege dhidi ya wasafiri wanaiongia na kutoka kwenye Mataifa hayo.
Kwa Mujibu wa Mochache ni kwamba watu wanaotoka kwenye Mataifa hayo watalazimika kupimwa na kuekwa Karantini kuambatana na sheria za afya licha ya kuwa na stakabadhi za kuonyesha kwamba wamechanjwa dhidi ya Corona.
Mochache aidha amewahimiza Wakenya kuendelea kuchanjwa kwa wingi akisema kwamba ndiyo njia pekee ya kukabili Mammbukizi zaidi.
Haya yanajiri wakati ambapo maambukizi mpya ya aina hiyo ya Corona ya Omicron yakiendelea kuthibitishwa katika Mataifa mbali mbali.
Virusi vya Omicron vilivyogunduliwa mara ya kwanza Nchini Afrika Kusini, sasa vimepatikana Nchini Uingereza, Ubelgiji, Australia, Ujerumani, Italia, India, Thailand miongoni mwa Mataifa mengine.