AfyaHabariNews

Mwanamke mwenye umri wa miaka 19 amejifungua mapacha walioungana katika kaunti ya Kisii.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 19 amejifungua mapacha walioungana katika hospitali ya Lenmek, eneo la Ogembo katika kaunti ya Kisii.
Mama ya mapacha hao, Lilian Moraa ambaye anatoka eneo la Kiong’ongi, Itumbe alifika hospitalini humo baada ya kutumwa kutoka hospitali ya Ogembo Level 4.
Daktari aliyeongoza shughuli ya kumsaidia mwanadada huyo kujifunguaEvans Monda, amesema kwamba mapacha hao wameunganishwa kuanzia kifuani hadi upande wa chini wa tumbo huku vipimo vya mapema vikiashiria kwamba viungo vingi vya watoto hao viko sawa.
Hata hivyo wamehitajika kupelekwa katika hospitali ya hali ya juu ili waweze kutenganishwa.