Baadhi ya wakaazi wa Mombasa hususan waliokuwa waajiriwa wa Bandari ya Mombasa KPA awali wamekana madai ya ripoti ya ukaguzi uliofanywa na kamati ya usawa katika bunge la seneti nchini kuwa idadi kubwa ya wafanyikazi wa bandari ya Mombasa ni jamii ya wamijikenda.
Akizungumza na kitengo chetu cha habari mwajiriwa wa zamani wa KPA David Mwatsuma, amesema kuwa nafasi nyingi za ajira zimepewa jamii zingine hivyo basi kuchangia jamii ya wamijikenda kukosa ajira katika banadari hiyo.
Aidha Mwatsuma ameongezea kuwa kunapotekea nafasi ya ajira Bandarini, wafanyikazi wa jamii zingine huchukuwana wao kwa wao, na kuwaacha nyuma wamijikenda bila kazi.
Wakati uo huo Mwatsuma ametowa wito kwa serikali iyangazie maisha ya jamii ya wapwani wasokuwa na ajira na iyache kuwabaguwa maana hata wao wana haki ya kuajiriwa.
BY NEWS DESK