HabariNewsSiasa

Vijana wahimizwa kujitosa katika masuala ya uongozi.

Baadhi ya viongozi ambao ni vijana ukanda wa pwani wamewahakikishia vijana wenza kwamba wanapojituma na kugombea nyadhifa mbalimbali nchini watapata asilimia kubwa ya uungaji mkono.
Akizungumza katika kipindi cha sauti asubuhi katibu wa utawala katika wizara ya teknolojia na mawasiliano Nadia Ahmed, amepinga vikali tetesi kuwa wazee ndio wanaopewa nyadhifa muhimu uongozini akisema kuwa rais Uhuru Kenyatta amepeana nafasi sawa kwa kila mwananchi.
Nadia aidha amewashauri vijana kupunguza starehe na kujituma zaidi kwani bidii yao ndio itakayochangia kwa wao kupatana nafasi za uongozi.
Aidha ametoa wito kwa vijana kufanya maamuzi ya busara wakati wa uchaguzi na kuepuka kutumiwa vibaya na viongozi wa kisiasa hasa wakti huu wa kampeni.

BY NEWS DESK