HabariNews

Afisa wa polisi amemuua mkewe na watu wengine watano kabla ya kujiua huko Kabete kaunti ya Kiambuu.

Afisa mmoja wa polisi eneo la Kabete kaunti ya kiambu amewauwa watu 5 kwa kuwapiga risasi na kisha kujiua kwa kujipiga risasi.
Hata hivyo inasemekana kwamba afisaa huyo wa polisi pia alimpiga mkewe risasi kabla ya kuondoka nyumbani mwendo wa saa 7 alfajiri.
kulingana na ripoti ya polisi ni kwamba jirani ya mwenda zake alisikia mlio wa risasi kabla ya kuwafamisha maasifa wa pilisi katika kituo cha polisi cha Kabete na baada ya kufika nyumbani walimpata mkeo afisaa huyo ameaga kufwatia kupigwa risasi.
Aidha OCPD eneo la Dagoreti amedhibitisha kisa hicho na kusema kwamba mmoja wa waathiria alikuwa ni mwendeshaji pikipiki ambae aliaga wakati akipokea matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta akiongeza kwamba kwasasa watu wawili wanaendelea kupokea matibabu.

BY NEWSDESK